Zimamoto Mbeya yawafikia wafanyabiashara sokoni na kutoa elimu ya kuzima moto
14 September 2023, 13:39
Elimu ni msingi wa kuongeza maarifa na ili uwe na amaarifa huna budi kuifunzz kwa waliofanikiwa kutkana na umhimu wa elimu jeshi la zimamoto haliko mbali na wananchi katika kuwapatia elimu pasipo kubagua rika,rangi,kabila wala umbo la mtu.
Na Ezra Mwilwa
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mbeya limebaini uwepo wa baadhi ya makundi ikiwemo masokoni kutokuwa na elimu ya vifaa vya kuzimia moto hali iliyopelekea kuyafikia makundi hayo na kutoa elimu.
Akitoa elimu katika soko la igawilo lilipo jiji Mbeya afisa habari wa jieshi nla zimamoto na uokoaji Coplo Ester Kinyaga amesema wanaowajibu wakuhakikisha kila mwananchi anafahamu matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto.
Katika hatua nyingine Coplo Ester amewataka wananchi kutoa taarifa ya pindi wanapoona matukio ya moto na mengine yanahitaji uokozi ikiwemo kudumbukia.
Nao baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Igawilo kutoka soko hilo wamelipongeza jeshi la Zimamoto kwakutoa elimu hiyo Pia wamesema walikua wakiona vifaa hivyo vimefugwa pasipo kujua matumizi yake.
Jeshi la zimemoto na uokoaji mkoa wa mbeya limekuwa na utaratibu wa kuwatembelea wananchi kwenye maeneo yao na kuwakusanya na kisha kutoa elimu kwenye mikutano ya hadhara.