Baraka FM
Baraka FM
12 September 2023, 11:11

Meneja wa radio Baraka Charles Amulike akiwa anatoa msaada wa vifaa vya shule katika shule ya msingi Ilota Mbeya vijijini (picha Hobokela Lwinga)
Vyombo vya habari vimekuwa vikiaminiwa kuwa na mchango wa kuibua changamoto mbalimbali katika jamii kutokana na hilo vinaoaswa kutumia wajibu wake kuwa chanzo cha kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Na Hobokela Lwinga
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilota Joel Munuo amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mwalimu wa kike kwa miaka kumi, upungufu wa madarasa, vyoo na nyumba za walimu.
akizungumza na kituo hiki Mwalimu Mkuu huyo amesema changamoto hiyo imekuwa ikisababisha wanafunzi wa kike kukosa huduma zinazoweza kutolewa na Mwalimu wa kike.
Hata hivyo Afisa elimu Kata ya Mshewe Yuda Kilawa amesema mchakato wa kumpata mwalimu wa kike ulikuwa unakwamishwa na ukosefu wa nyumba za walimu amesema kwasasa utakamilika kutokana na uwepo wa nyumba mbili walimu zilizojengwa.
Baada ya kupata uwepo wa changamoto hiyo kituo cha redio Baraka kimefika shuleni hapo na kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vifaa vya shule kama daftari.
Akizungumza kwa niaba ya kituo hicho cha redio meneja Charles Amlike amesema kazi ya chombo cha habari ni kuibua changamoto zinazoikumba jamii.
Nae Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilota Musa Jek ameupongeza uongozi wa Radio Baraka na wadau mbalimbali kwa kufanikisha tukio hilo.
Ipi Kauli Ya Wanafunzi Walipewa Msaada Huo….

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ilota wakifurahia zawadi za daftali walipewa na radio baraka