TADIO yawanoa wahariri, wataalam wa kidijitali mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
11 September 2023, 23:27
Katika kuimarisha na kupunguza changamoto zinazoikabili sekta ya habari nchini,TADIO imeendelea kuvijengea uzoefu vyombo vya habari ili kuondokana na mifumo ya analojia na kwenda kidijitali kulingana na mabadiliko ya ulimwengu.
Na Hobokela Lwinga
Wamiliki wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kutumia vyema mitandao ya kijamii ikiwemo kuhabarisha umma ili kuimarisha maendeleo ya kiuchumi ya taasisi zao.
Wito huo umetolewa na afisa mradi wa shirika la habari la maendeleo Tanzania Saum Bakari katika mafunzo yaliyowakutanisha wahariri na wakuu wa kidijitali kutoka mikoa mbalimbali ya Nyanda za Juu kusini yaliyoandaliwa na shirika hilo na kufanyika ktika ukumbi wa usungilo uliopo jijini Mbeya.
Bi. Saum amesema ili vyombo vya habari viweze kupata tija havina budi kutumia teknolojia kwani inasaidia kujitangaza.
Kwa upande wake mkufuzi kwenye mafuzo hayo Amua Rushita amesema mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo wasimamizi wa vyombo vya habari ili kuweza kujiongezea wafuasi ndani na nje ya mikoa yao.
Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo Lennox Mwamakula na Lusy Dashud wameahidi kwenda kuyafanyia kazi waliyofundishwa ikiwa ni pamoja na kuwezesha vyombo vyao kuanza kutumia fursa zilizopo kwenye mtandao wa TADIO.