Baraka FM

Moravian Mbozi yatoa ushirikiano wa utendaji Jimbo la Magharibi

26 November 2024, 05:49

Hawa ni viongozi mbalimbali katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika kanisa la Moravian ushirika wa Tunduma(picha na Deus Mellah)

Ili uwe Bora ni lazima ukubali kujifunza kwa wengine hii ndio maana halisi ya mafanikio katika nyanja mbalimbali katika maisha.

Na Deus Mellah

kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la magharibi Tabora wamefanya ziara ya kujifunza mfumo rafiki wa kuinua mapato ya ndani ya kanisa katika majimbo ya kusini, jimbo la kusini magharibi na jimbo la Mbozi.

Akizungumza na viongozi wa jimbo la mbozi katibu mkuu wa kanisa la moravian Tanzania jimbo la magharibi (Tabora) Mch Richard Rwali amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu wameona jinsi ya majimbo mengine wanavyoweka mchanganua wa makisio.

Viongozi wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Mbozi na jimbo la Magharibi( picha na Deus Mellah)
Sauti ya katibu Mkuu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Magharibi Tabora Mch Richard Rwali

Naye mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Magharibi wilaya ya kati Sikonge Benjemin Kamage amewaomba wakristo wa jimbo la Magharibi kukubali mfumo mpya wa mabadiliko na kupokea vitu vipya.

Baadhi ya waumini walio shiriki wakiwa katika Ibada ushirikani Tunduma(picha na Deus Mellah).
Sauti ya mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Magharibi wilaya ya kati Sikonge Benjemin Kamage

Kwa upande wake mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Mbozi Mch Lawrance Nzowa amewashukuru viongozi hao kwa kufanya ziara katika jimbo lao kwani wamebadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi katika kanisa.

Sauti ya mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Mbozi Mch Laulence Nzowa

Pia amewaomba wakristo wa jimbo la Mbozi kuendelea kuliombea kanisa na kuliombea taifa na viongozi wa nchi.

mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Mbozi Mch Lawrence Nzowa(picha na Deus Mellah)
Sauti ya mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Mbozi Mch Laulence Nzowa