🛑Breaking news,Gari ya kanisa la Moravian yapata ajali Chunya Mbeya
27 October 2024, 20:54
Wakati usambazwaji wa mitihani ya kidato cha pili ukiendelea kufanyika nchini changamoto imeweza kutokea katika halmashauri ya chunya.
Na Hobokela Lwinga
Watu kadhaa wamejeruhiwa katika ajali ya gari Mali ya kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi wilaya ya Chunya iliyotokea leo eneo la Chalangwa Chunya mkoani Mbeya.
Taarifa za awali inaelezwa kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 426 AJB iliazimwa na halmashauri ya Chunya kwa ajili ya kusambaza mitihani ya kidato cha pili inayotarajiwa kuanza kufanyika October 28,2024 nchini kote.
Aidha Majeruhi waliokuwemo kwenye gari hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha afya Chalangwa.
Jitihada za kumtafuta Kamanda polisi mkoa wa Mbeya ili kuthibitisha ajali hiyo zinaendelea, endelea kufuatilia Baraka Fm na kurasa zetu za mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi.