Baraka FM

Kanisa la Moravian laamuaga rasmi mch. Mbotwa

21 October 2024, 15:39

Kama ilivyo utaratibu wa kikatiba ya kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi kila mchungaji anayefikisha umri wa miaka 60 huwa anastaafu.

Na Deus Mellah

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusin Magharibi wilaya ya Mbeya limemuaga Mwenyekiti wao wa wilaya ya Mbeya Mch. Osia Mbotwa ambae amestaafu rasmi kulitumikia kanisa hilo.

Akizungumza katika ibada maalumu ya kumuaga Mch. Osia Mbotwa iliyofanyika katika kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi Ushirika wa Iyunga Askofu Robert Pangani amemshukuru Mch Mbotwa na familia yake kwa huduma waliyoifanya ndani ya kanisa.

Sauti ya Askofu kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi mchungaji Robert Pangani

Askofu Robert Pangani ameliomba kanisa hilo na Wachungaji wake kuwa na umoja na kupendana kwa maslahi ya maisha yao.

Askofu kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi mchungaji Robert Pangani
Sauti ya Askofu kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi mchungaji Robert Pangani

Naye Mch. Osia Mbotwa amesema amefanya kazi katika kanisa la Moraviani kwa miaka 41 na hajutii kufanya kazi katika kanisa hilo.

Sauti ya mchungaji Mch. Osia Mbotwa

Hata hivyo Mch Mbotwa amelishukuru kanisa kwa kumpa ushirikiano kipindi chote cha utumishi wake.

Mwenyekiti kanisa la Moravian wilaya ya Mbeya mchungaji Osia Mbotwa
Sauti ya mchungaji Mch. Osia Mbotwa

katika ibada hiyo kanisa kupitia michango ya waumini limeweza kumzawadia mchungaji huyo kiasi cha shilingi milion thelathini pamoja na chombo cha usafiri.