Baraka FM

Watahiniwa kidato cha nne 2024 watakiwa kujiandaa kwa bidii kufanya mtihani wa taifa

17 October 2024, 21:11

Baadhi ya wanafunzi wanaotarajia kufanya Mtihani wa kidato cha nne Shule ya Solace(picha na Deus Mellah)

Wakati wahenga wanasema elimu haina mwisho hii inamaana kwamba unapotoka hatua moja inakupeleka hatua nyingine ya elimu ya juu.

Na Deus Mellah

Wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mtihani wao wa taifa Novemba 11, 2024 wametakiwa kujianda na kupitia mara kwa mara yale waliyofundishwa na walimu wao ili waweze kufanya vizuri mtihani huo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa shule ya wasichana solace Roda Basili wakati akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo kuhusu wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao ilim waweze kufaulu mtihani huo wa taifa.

Mkuu wa shule ya wasichana solace Roda Basili( picha na Deus Mellah)
Sauti ya mkuu wa shule ya wasichana solace Roda Basili

Amesema kama walimu wa shule hiyo wanapambana ili kuhakikisha wanafunzi wa shule hiyo wanaoenda kufanya mtihani wanatimiza malengo yao.
Mmoja wa walimu shuleni hapo John Komba amewataka wanafunzi hao kuendelea kujifunza zaidi na tabia njema hapo watakapomaliza masomo yao ya kidato cha nne.

Mwalimu John Komba kutoka shule ya Solace(picha na Deus Mellah)
Sauti ya Mwalimu John Komba

Nao baadhi ya wanafunzi wamesema wamejianda sana na mtihani huo wa Taifa na wanahakikisha wanasoma kwa bidii.

Sauti za baadhi ya wanafunzi