Baraka FM

Jiji la Mbeya la tangaza urejeo wa mikopo ya asilimia 10

1 October 2024, 07:30

Wafanya biashara wadogo maarufu kama Machinga wametakiwa kutumia fursa za mikopo ya halmashauri na ile ya kimachinga inayo tolewa na serikali.
Wito huo umetolewa na Afisa Maendeleo Jiji la Mbeya Deus Mhoja katika mkutano na wamachinga kilichofanyika ukumbi wa shule ya samola jiji hapa kwalengo la kuelimisha juu ya mikopo ya asilimia 10%.

Sauti ya Afisa Maendeleo Jiji la Mbeya Deus Mhoja

Mhoja ameongeza kuwa kwa wale waliocbukua mikopo kabla ya kusitishwa watachukuliwa hatua za kisheria kama ilivyo ainishwa kwenye kanunu zamikopo hiyo.

Sauti ya Afisa Maendeleo Jiji la Mbeya Deus Mhoja akieleza kuwachukulia hatua ambao hawaja rejesha mikopo

Nae mwenyekiti wa Machinga mkoa wa Mbeya Jerry Mwatebela amewaomba wafanya biashara hao kutumia fursa hiyo pia amewataka wasijiingize kwenye maswala ya vurugu kutoka na changamoto wanazo kutanazo.

Sauti ya mwenyekiti wa machinga mkoa wa Mbeya

kwaupande wake mwenyekiti wa Machinga jiji la ndugu Waziri Hemed amesema wamaachinga wahakikishe wanashiriki uchaguazi nayeye kama kiongozi atatumia kipindi hicho kupigania haki za wamachinga.

Sauti ya mwenyekiti wa Machinga jiji la ndugu Waziri Hemed

Baadhi ya washiriki katika mkutano huo Anastazia Kyamba na Mbushi Shitindi wametoa shukrani zao kwakutanishwa na kupewa Elimu.

Sauti za Baadhi ya washiriki