Wahitimu vyuo vya Biblia watakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani nchini
17 December 2024, 15:14
Inawezekana ulikuwa unafahamu kuwa elimu ya kawaida ndiyo inapata nafasi ya kufanyiwa mahafali tu,sasa unapaswa kujua kuwa hata elimu ya Kiroho nayo inafanyiwa mahafali.
Na Deus Mellah
Wachungaji wanaohitimu masomo yao katika vyuo mbalimbali vya Biblia katika ngazi mbalimbali wametakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kuhimiza umuhimu wa imani ya nchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Wito huo umetolewa na katibu wa chuo cha bibilia cha A.M.O internation Bible college Robert Mwashiuya wakati akizungumza na wachungaji waliohitimu masomo ya Biblia katika chuo hicho.
Amesema kuna umuhimu mkubwa wa wachungaji hao kuwa mstari wa mbele katika kudili na jamii na kudumisha amani katika taifa la Tanzania .
Naye miongoni mwa wakufunzi wa chuo hicho Rememba Amon amewataka wachungaji hao kuhakikisha wanayatendea kazi yale yote waliyofundishwa katika chuo hicho.
Kwa upande wake Askofu.Mwaisabila amesema kuwa kazi ya uchungaji ni kazi ya kujitolea hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha wachungaji hao wanafanya kazii kwa bidii.
Nao baadhi ya wachungaji wanafunzi waliohitimu masomo yao katika chuo hicho wameahidi kuwa kielelezo katika jamii kwa kufundisha kweli ya Mungu.