Wakristo watakiwa kushiriki mikutano ya Injili
29 October 2024, 19:24
Mikutano ya injili ambayo imekuwa ikifanyika maeneo mbalimbali imekuwa na matokeo chanya hali hiyo imekuwa ikisaidia kuhamasisha watu kuishi kwa amani na upendo.
Na Iman Anyigulile
Waumini wa dini ya kikristo mkoani Mbeya wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mikutano ya injili inayo itishwa na watumishi wa Mungu kwa lengo la kufundisha neno la kweli.
Hayo yameelezwa na mchungaji David Mwazembe wa kanisa la RGC Victory church Mbalizi wakati akizungumza na kituo hiki kuhusu maandalizi ya mkutano wa injili unao tarajiwa kuanza 30 october hadi tarehe 3 November, 2024.
Mchungaji Mwazembe amesema lengo la kuandaa mkutano huo ni kuwatafuta watu wote walio potea na kuwafundisha injili iliyo ya kweli ya kuwaokoa na maovu.
kwa upande wake mchungaji Prince Paul kutoka Dares saalaam muhubiri wa mkutano huo amesema wao kama watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwafikia watu mbalimbali.