Baraka FM

Kijana anusurika kifo tuhuma za kuiba pikipiki Mbeya

8 October 2024, 07:40

Hali ya mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki baada ya kukamatwa

Ili kuondokana na uhalifu kwenye jamii, wananchi wamekuwa wakishauriwa kuwa na bidii ya kufanya kazi.

Na Ezekiel Kamanga

Kijana mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi amenusurika kifo baada ya kupigwa baada ya kutuhumiwa kuiba pikipiki ya Chama Cha Mapinduzi inayotumiwa na kada Shaban Kilosa tukio lililotokea eneo la uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mohamed mashango ni mwenyekiti mstaafu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya amesema alibaini pikipiki hiyo kuibiwa baada ya kuona iko na mtu asiyemfahamu ndipo alipo muuliza anapeleka wapi baada ya kuuliza mtuhumiwa huyo alianza kukimbia.

Kwa upande wake kada wa CCM Shabani Kilosa amesema alipaki pikipiki hiyo baada ya kutoka kwenye kikao huku akisema mwizi huyo ameharibu chombo hicho kwa kukatakata nyaya mbalimbali.

kada wa CCM Shabani Kilosa ambaye ndiye anatumia pikipiki hiyo ya chama

Wakizungumzia tukio baada ya kutokea baadhi ya mashuhuda wamesema watu hao wanaofanya vitendo hivyo wanarudisha nyuma maendeleo ya watu.

Taarifa za awali zinadai kijana huyo anajihusisha na matukio ya wizi Mkoani Mbeya.