Baraka FM

Sekondari mpya Mufindi kupewa huduma za maji,umeme

4 October 2024, 13:09

Naibu waziri wa viwanda na biashara na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini mhe.Exaud Kigahe

katika kuweka Mazingira mazuri ya elimu Jamii inapaswa kushiriki kikamilifu katika kujenga ustawi Bora wa elimu nchini.

Na Rukia Chasanika,Mufindi Iringa

Naibu waziri wa viwanda na biashara na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Exaud Kigahe ameahidi kuweka maji na umeme katika shule ya sekondari Mufindi ili wanafunzi waweze kusoma nyakati za zote.

Hayo yamesemwa na mgeni rasmi katibu elimu,Malezi na mazingira wa jumuia ya wazazi chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi John Mgina akimwakilisha naibu waziri na mbunge wa Mufundi kaskazini katika mahafari ya kwanza ya shule ya sekondari Mufindi iliyopo mkoani Iringa.

Mgeni rasmi katibu elimu,Malezi na mazingira wa jumuia ya wazazi chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi John Mgina(picha Rukia Chasanika)
Sauti ya mgeni rasmi katibu elimu,Malezi na mazingira wa jumuia ya wazazi chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi John Mgina

Katibu Mgina amesema mbunge huyo baada ya kupokea maoni kwa wananchi juu ya umbali wa shule ya sekondari kwa watoto waliamua kuanza mchakato wa kujenga sekondari mpya ambayo ilipewa jina la Mufindi ili wanafunzi wasome karibu na nyumbani kwao.

Sauti ya mgeni rasmi katibu elimu,Malezi na mazingira wa jumuia ya wazazi chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi John Mgina

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondary Mufundi Anitha Mbilinyi amesema wanafunzi wanaohitimu kwa mara kwanza katika shule hiyo ni 36 wavulana 12 na wasichana 24 ambao walihamia wakiwa kidato cha tatu kutoka sekondari ya Ifwagi.

Sauti ya mkuu wa shule ya sekondary Mufundi Anitha Mbilinyi

Afisa mtendaji wa kata ya Ikongosi Deogratias Lugenge amemshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Kigahe kwa kutoa fedha kiasi cha sh milioni mia sita sitini na tano kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.

Sauti ya afisa mtendaji wa kata ya Ikongosi Deogratias Lugenge