Baraka FM

Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi jiji la Mbeya wajengewa uwezo

30 September 2024, 15:34

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakila kiapo(picha na Deus Mellah)

Maandalizi kuelekea uchaguzi wa serikali mitaa ambapo tayari elimu imeanza kutolewa kwa wasaidizi wa wasimamizi wa uchaguzi huo.

Deus Mellah

Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuhusu kanuni na taratibu za kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo msimamizi msaidizi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Davis Mbembela amewataka wasimamizi hao kuzingatia yote wanayoelekezwa na kuwa wawazi.

Sauti ya msimamizi msaidizi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Davis Mbembela

Mbembela ameongeza kuwa wasimamizi hao watapitishwa kwenye maeneo ya uchaguzi ili wayafahamu sambamba na kuwajua wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.

Msimamizi msaidizi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Davis Mbembela(Picha na Deus Mellah)
Sauti ya msimamizi msaidizi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Davis Mbembela

Naye Ally Nunduma ambaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi halmashauri ya jiji la Mbeya amesema wanaendesha mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili wananchi wapate elimu.

Sauti Ally Nunduma ambaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi halmashauri ya jiji la Mbeya

Amesema katika jiji la Mbeya kuna tarafa mbili, kata thelathini na sita na mitaa miamoja themanini na moja ambapo chaguzi huo utafanyika.

Sauti Ally Nunduma ambaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi halmashauri ya jiji la Mbeya

Akizungumza kwa niaba ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi waliopata mafunzo hayo Liliani Mwakitosi amesema watafuata kanuni na sheria za uchaguzi ambazo zimewekwa pamoja na kutenda haki kwa wananchi wote.

Sauti ya mmoja wa washiriki wa mafunzo Liliani Mwakitosi