Baraka FM

Wanahabari Mbeya, Iringa na Njombe wajengewa uwezo

21 September 2024, 07:07

Wengi wa Watu wamekuwa na mazoea ya kufanya kazi Bila kutafuta maarifa mapya kuhusu kazi wanazozifanya,hata hivyo baadhi ya Watu wamekuwa wakipuuza pale tu fursa ya mafunzo inapokuwa imejitokeza kwa visingizio mbalimbali ikiwemo wingi wa majukumu.

Na Hobokela Lwinga

Imearifiwa kuwa Mkoa wa Mbeya umepokea fedha za maendeleo kiasi Cha shillingi trillion 1.6 kwajili ya kukamilisha Miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw.Beno Malisa ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera Wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya wadau wa vyombo Vya habari yaliyojumuisha mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe yaliyofanyika jijini mbeya.

Malisa Amesema kwamba kila sekta imeweza kuguswa ili kuondoa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wananchi ikiwemo katika sekta ya elimu, Afya, miundombinu ya barabara, maji, Usafiri wa anga, kilimo pamoja na nishati.

Rose Ruben ni mkurugenz mtendaji wa TAMWA amesema mafunzo hayo yamehusisha kada mbalimbali katika tasnia ya habari ikiwemo, wahariri,mameneja wa vyombo Vya habari, waandishi wa habari, waandaaji wa maudhui mtandaoni pamoja na watangazaji kutoka katika mikoa hiyo.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamewashukuru TAMWA na TCRA kwa kuandaa mafunzo hayo wamesema elimu hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao huku wakiahidi kwenda kufanya kazi kwa weledi unaotakiwa.