Wafugaji Mbeya wampongeza Dkt.Samia kwa uchapakazi wake wa vitendo
5 September 2024, 22:54
Katika kuondoa migogoro kati ya wafugaji na wakulima Serikali Imeendelea kuwa karibu na makundi hayo kujua changamoto ambazo wanakabiliana nazo ili ziweze kutatuliwa.
Na Hobokela Lwinga
Chama Cha mapinduzi kupitia Serikali yake inayongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Dkt.samia suluhu Hassan kimeahidi kutatua kero zote za wafugaji Kama ambavyo kimeendelea kutatua changamoto hizo katika sekta zingine.
Akizungumza na wafugaji katika kongamano la kumpongeza Rais Samia lililoandaliwa na chama Cha wafugaji mkoa wa Mbeya, Mjumbe wa halmashauri kuu chama Cha mapinduzi taifa mkoa wa Mbeya ndugu Ndele Mwaselela amesema serikali ya CCM ni sikivu.
MNEC Mwaselela amesema yapo mambo mengi Rais Samia ameyafanya kwa wafugaji hao ikiwa ni pamoja na kutengeneza majosho na kutoa dawa za kuogeshea mifugo bure.
Hata hivyo mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Mbeya Noah Mwakisu amewataka wafugaji hao kutumia fursa zinazotolewa na mwenyekit wa CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Huku akisema ni mtetezi wa makundi yote.
Akisoma risala kwa niaba wafungaji Mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Mbarali Phillip Oyeelayi Kaneyi amesema kero yao kubwa ni uhaba wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya wafugaji maeneo mbalimbali hasa katika halmashauri ya Mbarali.
Kwa upande wao baadhi ya wafungaji wameishukru serikali kwa kuendelea kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili.
Aidha katika kongamano hilo Ndugu Ndele Mwaselela amekubali kuwa mlezi wa wafugaji mkoa wa Mbeya baada ya ombi hilo kuwasilishwa na mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Mbarali ndugu Phillip Oyeelayi Kaneyi.