Taharuki sekondari Mbeya day kisa mzungu kugawa biskuti
2 September 2024, 19:01
Wakati serikali na jamii kwa ujumla ikipambana na mmonyoko wa maadili unaosababisha masuala ya ushoga kwa vijana wengi baadhi ya watu wamekuwa wakipuuza Hali hiyo inajitokeza katika moja ya shule Mbeya ambapo mtu asiyefahamika amebainika akigawa biskuti zinazodhaniwa kutokuwa salama.
Na Hobokela Lwinga
Taharuki na sintofahamu imeibuka katika shule ya sekondari ya Mbeya Day jijini Mbeya baada ya kuibuka kwa raia wa kigeni ambaye jina lake halijfahamika kugawa biskuti kwa wanafunzi wa shule hiyo huku walengwa wakuu wakiwa wasichana ambao wamefikia hatua ya kupevuka.
Wakizungumzia suala hilo wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya day wamedai kuwa baada ya kuona mzungu huyo anazunguka katika Mazingira ya shule huku akigawa biskuti bure akiwa amewalenga zaidi wanafunzi wa kike waliamua kutoa taarifa kwa Mkuu wa shule hiyo.
Hata hivyo Mkuu wa shule hiyo ya Mbeya day mwalimu Francis Mwakihaba amesema baada ya kupata taarifa hiyo walitoa taarifa kwa viongozi ngazi za juu na kisha kuweka ulinzi na mtengo wa kumnasa mzungu huyo lakini bahati mbaya hawajafanikiwa kumkamata kwani aligundua na kutokomea kusiko julikana.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amewataka wanafunzi hao kujiepusha kupokea zawadi kwa watu wasio wafahamu.