Mbeya Dc kinara uzalishaji zao la Pareto nchini
1 June 2024, 07:15
Pareto ni zao la biashara linalotumika kutengenezea viuatilifu mbalimbali vya kuua wadudu wanao tambaa na kuruka.
Na Hobokela Lwinga
Mkuu wa wilaya ya Mbeya mhe.Beno Malisa amesema mnunuzi yeyote ambaye atakiuka miongozo katika katika kununua zao la pareto atachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na mawakala wa makampuni husika.
Mkuu huyo ameyasema hayo katika Kikao kazi cha wadau wa zao la Pareto kuhusu umhimu wa kufuata sheria na kanuni zao la pareto kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa GR comfort kabwe jijini Mbeya.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ameyataka makampuni yote ya ununuzi wa Pareto katika halmashauri ya Mbeya kulipa kodi na atakaye kiuka mkono wa sheria utachukua mkondo wake.
Awali akizungumza mkurugenzi mkuu bodi ya Pareto nchini Lucas Kiayo amesema halmashauri ya Mbeya ndiye kinara wa uzalishaji wa zao la pareto ambapo ni asilimia 85 pareto inazalishwa katika halmashauri hiyo.
Afisa kilimo na mifugo halmashauri ya Mbeya Gidion Mapunda amesema kwa sasa wanunuzi wote wanapaswa kufuata mashariti ya ununuzi ikiwa ni pamoja na kununua kwenye vituo mahususi sambamba na kutokununua pareto mbichi.
Baadhi ya wadau wa kilimo cha pareto na wanunuzi wa zao hilo Gerald Joseph kutoka PCT na Musa mnasi SHANATEC LIMITED wameiomba serikali kuingilia kati kilimo cha Pareto ili kiendelee kuzalishwa kwa ubora.