Baraka FM

Wahitimu wa vyuo tumieni fursa zinazojitokeza

20 May 2024, 10:38

Baadhi ya wanafunzi wa makanisa ya CCT chuo kikuu Teofilo Kisanji wanatarajia kuhitimu masomo yao mwaka huu(picha na Ezra Mwilwa)

Kufuatia soko la ajira linalo endelea hapa Nchini kuwa finyu wahitimu wanapaswa kutafuta njia mbadala wa kujiajiri.

Na Ezra Mwilwa

Wanafunzi wanaoelekea kuhitimu masomo ya vyuo wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza bila kujali tahasusi walizozisomea vyuoni.

Wito huo umetolewa na Mch. Kubadima Misugwi katika mahafali ya wanafunzi wa makanisa ya CCT Chuo Kikuu Teofilo Kisanji ambapo amesema vijana wengi wanashidwa kufikia malengo yao ya maisha kwa kuchagua fursa zinazojitokeza katika jamii pia kutotumia vipaji vyao.

Mchungaji Kubadima akiwaasa wahitimu chuo kikuu Teofilo Kisanja jjijini Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)

Nao baadhi ya wahitimu wameahidi kuhakikisha wanatimia ujuzi na Elimu waliyo ipata kujikwamua kiuchumi bila kutegemea ajira pekee.

Wanafunzi wanaotarajia kuhitimu masomo yao mwaka huu 2024 chini ya makanisa ya CCT chuo kikuu Teofilo Kisanji(picha na Ezra Mwilwa)

Aidha mwenyekiti wa Umoja huo Obed Seme amesema wahitimu hao waendelee kumtumikia Mungu na kuishi katika kusudi la Mungu.