Watu kadhaa wahofiwa kwa kufa ajali Mbeya
6 May 2024, 18:08
Watumiaji wa barabara wamekuwa wakisisitizwa kutii na kufuata sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima sambamba na kukagua vyombo vyao kabla ya safari.
Na Hobokela Lwinga
Watu kadhaa wanahofia kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali ya roli lililokuwa limebeba mzigo wa mchele baada ya kufeli break lenye usajili wa T 422 AKF lililokuwa likivuta tela T 393 APE aina ya scania katika eneo la mbembela kata ya nzovwe barabara kuu ya Zambia mbeya.
Wakizungumzia ajali hiyo baadhi ya mashuhuda wamesema dereva wa gari hiyo alianza kuomba msaada na kutoa taarifa ya hatari baada ya kuwasha taa.
Aidha Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mrakibu wa jeshi la polisi Hussen Gawile amewataka madereva kuchukua tahadhali wakati wa uendeshaji wa vyombo vya moto sanjari na kuheshimu alama za barabara.
Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Abdi Issango amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema wanamshikilia derava wa roli kwa kosa la kutokuzingatia alama za barabarani.
Majeruhi katika ajali wanaendelea kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya.