T.A.G Galilaya laadhimisha miaka 85 kwa kupanda miti
23 April 2024, 11:42
Utunzaji wa mazingira hautegemei mtu mmoja au kikundi fulani bali utunzaji wa mazingira unamtegemea kila mtu kutokana na kwamba kila kiumbe hai kinategemea mazingira safi na bora katika eneo alikopo, zipo athali mbali ambazo zinaweza kujitokeza katika uharibifu wa mazingira ikiwemo athali za mabadiliko ya tabia ya nchi kama vile mafuriko na hata ukame.
Na Iman Anyigulile
katika kuadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa kanisa la Tanzania Assemblies of God kanisa la Tanzania asemblies of God Galilaya airport wamefanya zoezi la kupanda miti na kufanya usafi katika kituo cha afya cha kata ya iyela jijini mbeya.
Wakiwa kituoni hapo waumini wa kanisa hilo wamesema kutokana na maadhimisho hayo wameamua kutoa hamasa kwa wengine kwa ajili ya kufika kwenye kituo hicho na kuweza kujitolea kwa chochote ambacho kitakuwa msaada kwa wengine .
kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya uinjilisti na umission ndani ya kanisa la T. A. G Galilaya William Mwamole amesema kuwa wao kama kanisa wameamua kufanya shughuli za kijamii hasa kwa kufanya usafi katika kituo cha afya kata ya Iyela.
Nae mchungaji wa kanisa hilo Joseph Harembo amesema maadhimisho hayo ya miaka 85 ya kanisa hilo wameamua kupanda miti 40 ya matunda na vivuli kwa ajiri ya mazingira ya kituo hicho.