Dc Batenga; Wanafunzi Chunya mna deni la kulipa kwa Rais
27 February 2024, 19:45
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa UhamiajI Mhe. Mubaraka Alhaji Batenga amesema kuwa wanafunzi wilaya ya Chunya wana deni kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa matokeo ya mahusiano mazuri aliyoyajenga na Nchi zingine hali inayopelekea kupata wafadhili kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu kwa kuhakikisha Miundombinu inajengwa kurahisisha upatikanaji wa Elimu
Mhe. Batenga ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Itewe lililojengwa kwa asilimia themanini ya fedha (80%) ya fedha kutoka taasisi ya Foundatio for Education to Improve Family Planning (FEFP) kupitia Cocoa for schools.
Kupatikana kwa wafadhili hawa ni matokeo ya mahusiano mazuri ya Tanzania na Mataifa mengine lakini anayeanzisha na kuimarisha mahusiano haya namba moja ni Mhe.Rais mwenyewe na sisi wengine tunafuata kwahiyo ninyi wanafunzi wa Itewe na wilaya ya Chunya mnadeni kwa Mhe. Rais
Aidha Mhe Batenga ametoa rai kwa wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii masomo ya Sayansi lakini pia waongeze juhudi katika kujifunza Lugha ya Kiingeleza ili waweze kuwasiliana na wageni kutoka mataifa mengine na miundombinu yote ya kufanikisha hayo imejengwa na Serikali ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ili wanafunzi wote wanufaike
Naye mwanzilishi wa Shilika la Cocoa For Schools ndugu Fons Maex amewaasa wanafunzi kuto kujihusisha katika mahusiano ili kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea ikiwa ni pamoja na mimba za utotoni ambazo zitasababisha kuzima ndoto zao za hapo badae.