St. Francis Mbeya wafanya maombi kabla ya mtihani kidato cha nne
13 November 2023, 15:48
Na Deus Mellah
Wakati mtihani wa taifa wa kidato cha nne ukianza leo kwa shule zote za sekondari nchini wanafunzi kidato cha nne wa shule ya St. Francis girls ya jijini Mbeya wamefanya ibada maalumu ya kumuomba Mungu ili aweze kuwasaidia kufanya vizuri katika mitihani hiyo.
Wakizungumza na kituo hiki katika ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi ushirika wa Ruanda wamesema mtihani wa taifa wa kidato cha nne ndio muongozo wa maisha yao hivyo ni jambo la msingi kumtegemea Mungu.
Mmoja wa wanafunzi hao Yunislois Spaika amesema kuwa wao kama wanafunzi wamejianda vizuri katika mtihani huo wa taifa wa kidato cha nne
Naye Faraja Chanila amewaomba wanafunzi wengine wanaofanya mithani leo kuendelea kumwamini na kumtegemea Mungu pekee katika mtihani huo.
Kwa upande wake mch Jamson Mwiligumo mwalimu wa shule ya St.Francis amewataka wanafunzi mbalimbali wanaofanya mitihani kuwa watulivu katika chumba cha mtihani.
Pia amewaomba wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele katika kuwaunga mkono watoto wao wanaofanya mtihani ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.
Ikumbuke kuwa mtihani wa taifa wa kidatio cha nne umeanza novemba 13,2023 katika shule zote za sekondari nchini.