Uhasibu ndaki ya Mbeya yazalisha wahitimu Zaidi ya 2000 kada mbalimbali
3 November 2023, 22:58
Jumla ya wahitimu elfu mbili mia moja kumi na nne wa kada mbalimbali za Taasisi ya Uhasibu Ndaki ya Mbeya wametunukiwa vyeti vyao ikiwa ni Mahafali ya ishirini na moja nchini na ya kumi na moja kampasi ya Mbeya mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera.
Na Hobokela Lwinga
Mkuu wa Mkoa Wa Mbeya Comrade Juma Homera Leo Novemba 3 2023 ameshiriki Mahafali ya 11 ya Chuo Cha Taasisi ya Uhasibu TIA Ndaki ya Mbeya ambapo amewaasa Wahitimu mara warudipo Uraiani wawe sehemu ya Utatuzi wa hoja zenye Changamoto na si waanzilishi wa hoja hizo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera Amesema Serikali inaendelea kuwaunga Mkono Wanafunzi kuhakikisha wanatimiza Malengo na Ndoto zao ambapo Zaidi ya fedha Bilioni 731 zimetengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt: Samia Suluhu Hassan kwaajiri ya kuwawezesha Mikopo Wanafunzi wa Vyuoni kama ambavyo Mwaka 2022-2023 zaidi ya Bilioni 646 zilitolewa kwa Wanafunzi 73500.
Aidha RC Homera ameipongeza Serikali kwa Mikakati Bora ya kuwawezesha Wanafunzi kielimu hasa kwa kutoa kipaumbele kwa Wanawake.
Katika hotuba yake Homera amesema Taasisi ya Uhasibu Mbeya imevunja rekodi kwa kuwa na wahitimu wengi wanawake.
Said Msendo ni mwakilishi wa Bodi kutoka Wizara ya fedha amesema ushahidi mkubwa wa malengo umeongeza idadi ya wahitimu.
Afisa Mtendaji Mkuu William Palanjo amesma kukamilika kwa jengo jipya Taasisi ya Uhasibu Mbeya kutaongeza idadi ya wanachuo.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tawi la Mbeya Merikio Akyo amesema Chuo kinaendelea kuwapa fursa ya ubunifu wanachuo wake.
Wahitimu wengi hivi sasa wameacha kutegemea ajira kutokana na mbinu bora wanazofundishwa na wakufunzi wao hivyo kuondokana na dhana ya kuajiriwa.