LATRA yatoa msimamo wa upandaji wa nauli za daladala Mbeya
14 October 2023, 06:16
Madereva mbeya wamekuwa na mgomo ambao umepelekea changamoto ya ukosefu wa usafiri,na baadhi ya wahudumu kuwatoza abria nauli ya shilingi 700 kutoka mbalizi hadi kabwe tofauti na nauli ya awali ya shilingi 500.
Mamlaka Ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA mkoa wa Mbeya imewataka madereva wa mabasi ya abiria kuacha kupandisha nauli kinyume na utaratibu kwa kuwa ni kosa kisheria.
Hayo yameelezwa na meneja wa mamlaka hiyo ndugu Omary Ayubu wakati akizungumza na kituo hiki baada ya kupokea malalamiko ya abiria kuhusu baadhi ya madereva kupandisha nauli kutoka shingi mia tano hadi mia saba.
Ayubu amesema kwa sasa nauli ambayo abiria anapaswa kulipa ni shilingi mia tano kwa kituo hadi kituo na endapo kutakuwa na mabadiliko basi taarifa kamili zitatolewa.
Nae Said Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa vyombo vya usafiri Ardhini mkoa wa Mbeya amesema wao kama baraza hawajapokea malalamiko kutoka kwenye uongozi wa umoja wa madereva hivyo wanawaomba wafuate sheria.