DSW yatoa mafunzo kwa Vijana,walimu na watalaamu wa afya chunya
6 December 2024, 18:47
katika kuhakikisha sauti za vijana zinasikika ili kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuwapatia huduma rafiki kwa afya ya vijana viongozi wa shirika la DSW Tanzania wamewakutanisha vijana,walimu na wataalamu wa afya Chunya mkoani Mbeya.
Na Lukia Chasanika
Vijana,walimu na wahudumu wa afya wametakiwa kuzingatia mafunzo yanayotolewa na shirika la DSW Tanzania kupitia mradi wa REST ili kuyatumia kuelimisha jamii inayowazunguka.
Hayo yamesemwa na afisa elimu vifaa na takwimu sekondari wilaya ya Chunya Costancia Komba akimwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chunya wakati akifungua mafunzo kwa walimu na vijana yaliyaandaliwa na shirika la DSW Tanzania kupitia mradi wa REST.
Aidha mkurugenzi wa shirika la DSW Tanzania Peter Owaga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia mafunzo washiriki kuimarisha mifumo iliyopo na kuhakikisha sauti za vijana zinasikika ili kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuwapatia huduma rafiki kwa afya ya vijana.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya vijana Joseph Sunge amelishukru shirika hilo kwa kupeleka mradi wa REST katika wilaya ya Chunya hususani tarafa ya Kipembawe ambako vijana wengi wapo katika mashamba ya tumbaku.
Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo kitaifa katika huduma rafiki kwa vijana Mariam Mhanjim amesema wanatoa mafunzo kwa watoa huduma namna ya kutoa huduma rafiki kwa kijana kulingana na mahitaji yao.
Baadhi ya vijana walioshiriki katika mfunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi katika huduma mbalimbali za kijamii katika kata zao walizotoka za wilaya ya chunya.