Baraka FM

Jamii imetakiwa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu

17 October 2024, 15:43

Baadhi ya familia walipokea msaada kutoka Iyela Mamas (picha Flora Godwin)

Kumekuwa na familia nyingi zinazoishi katika hali duni za maisha kwa kutambua hilo kila mtu anawajibu wa kusaidia jamii hizo ili kuondokana na changamoto zinazozikabili.

Na Flora Godwin

Kikundi Cha Iyela Mamas wameto msaada kwa wahitaji zaidi ya 50 wakijumuishwa wazee, wajane na watoto yatima.

Akizingumza na kituo hiki mwenyekiti wa kikundi hicho Scora Asei amesema Group hilo linajumla ya wanafamilia 106 na lengo lao ni kuhudumia watu wenye uhitaji maalumu lakini pia wamekuwa na malengo ya kuwaandaa watoto wakike kuwa viongozi bora wa baadae.

Lakini pia ameviomba baadhi ya vikundi vinavyo jihusisha na mambo ya kijamii kuzingatia pia wahitaji walioko majumbani sio kuwahudumia wale tu wanaopatikana katika maeneo maalumu.

Sauti ya mwenyekiti wa kikundi hicho Score Asei

Kwa upande wake Zamira Muihojo ambaye ni katibu wa Iyela Mamas amewashukuru wanachama wa kikundi hicho kwa namna walivyojitolea kwa wahitaji hao.

Sauti ya karibu wa Iyela mamas Zamira Muihojo

Nao wanachama wa Iyela Mamas wanawashukuru viongozi wao kuwa na maono bora na yenye tija kwenye kundi lakini pia kwa jamiii inayo wazunguka.

Sauti za radhi ya wanachama wa Iyela Mamas Mbeya

Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya wahitaji hao wamewashukuru wanafamilia hao kwa upendo wa dhati walio uonyesha kwa upendo wao.

Sauti za baadhi ya watu wenye uhitaji wakishukru.

Elisha Pita ni afisa mtendaji wa mtaa wa Iyela One amesema kikundi hicho kimekuwa msaada mkubwa kwenye jamii nakutaka baadhi ya vikundi kuiga mfano huo.

Sauti ya Elisha Pita ni afisa mtendaji wa mtaa wa Iyela One