Chuo kikuu TEKU chafanya ibada ya kumshukru Mungu
20 February 2024, 10:38
Na Ezra Mwilwa
Kanisa la Moravian Tanzania Ushirika wa Teku wamefanya Ibaada maalumu kwaajiri ya kumshukuru Mungu juu ya Chuo kikuu Teofilo Kisanji kuendelea kukua na kutunukiwa hadhi kubwa ya vyuo vikuu Nchini.
Katika ibada hiyo imehudhuriwa na Askofu Mteule wa Kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi Mch. ROBART PANGANI amesema anawapongeza washirika wa Teku kwakuendelea kukiombea chuo panoja na viongozi wake.
Nae mkuu wa chuo Prof. HERIMAS MWANSOKO amesema chuo kimepandishwa rasmi katika hadhi ya vyuo vikuu hapa mchini na kuwaomba wa moravian kuendelea kukipa kipaombele chuo hicho.
katika ibada hiyo iliandaliwa Risala iliyo eleza dhima ya Ibada hiyo na kusomwa na Wakili wa Ushirika Dkt. Gwamaka Mosespia Mchungaji wa ushirika Mchungaji DUNCAN MWALYOLO amesema wakristo waendelee kukiombea chuo hicho pamoja na taasisi zote za kanisa.
Ibada hiyo imehudhuriwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi ikiongozwa na MUSSA AMON ambaye amesema wanamshuru Mungu kwakuendelea kuona wanafunzi wanaongezeka ndani ya chuo.