Hospitali ya rufaa Mbeya yatoa mafunzo kwa watumishi wa wagonjwa wa dharula ICU
23 January 2024, 09:06
Na mwandishi wetu
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Bi Myriam Msalale, leo amefungua rasmi mafunzo ya msingi ya huduma za dharura kwa watumishi wa wodi maalum ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo na kuongeza ujuzi watumishi hao katika kutoa huduma bora na ya kina kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu.
Msalale amesema hospitali hiyo ya Rufaa Mbeya inatambua umuhimu wa kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa katika hali mbaya, na kwa hiyo itaendelea kuwekeza katika mafunzo ya kudumu kwa watumishi wa wodi ya ICU.
Amesema wataboresha ujuzi na maarifa yao, watoa huduma hao wataweza kukabiliananna changamoto pamoja ma kupata mbinu mpya za matibabu ilikuokoa maisha ya wagonjwa.
Kaimu Mkurugenzi Msalale ametoa wito kwa watumishi wote wa wodi ya ICU kushiriki kikamilifu katika mafunzo haya na kuchukua fursa ya kuendeleza ujuzi wao.
Pia, amewaahidi kuendelea kutoa mazingira bora ya kujifunza ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata huduma bora wanapohitaji.