Zenj FM

Mtalii mmoja, mti mmoja Zanzibar yawasha kampeni ya kurejesha uoto wa asili

28 November 2026, 22:35

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Suleiman Masoud Makame akiwa na viongozi wa OTESHA na wadau wa utalii Zanzibar wakipanda mti ikiashiria kuzindua kampeni ya kuwashirikisha watalii katika upandaji wa miti, zoezi lililofanyika katika bustani ya Forordhani Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha kampeni ya kuwashirikisha watalii katika upandaji miti, ikilenga kupanda hadi miti 200,000 kwa mwaka ili kurejesha uoto wa asili, kulinda mazingira na kuifanya Zanzibar kuwa ya kijani zaidi.

Na Mary Julius

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezindua kampeni ya upandaji miti ya “Visit Zanzibar, Make It Greener” kwa lengo la kurejesha na kuimarisha uoto wa asili pamoja na kuifanya Zanzibar kuwa ya kijani.

Akizindua kampeni hiyo katika bustani ya Forodhani, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Suleiman Masoud Makame, amesema ushiriki wa watalii katika upandaji miti unaweza kusaidia kupanda takribani miti 200,000 kwa mwaka.

Amesema Serikali imesaini makubaliano na taasisi ya OTESHA ili kuimarisha ushirikiano wa uhifadhi wa mazingira, huku akiwataka wadau wa utalii na wananchi kushiriki katika upandaji na utunzaji wa miti.

Sauti ya Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Suleiman Masoud Makame.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa OTESHA Zanzibar, Rumisho Shikonyi, amesema taasisi hiyo inalenga kupanda na kutunza miti 50,000 ndani ya siku 30, kuanzia Desemba Mosi hadi 31 mwaka huu.

Sauti ya Mkurugenzi wa OTESHA Zanzibar, Rumisho Shikonyi,

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira, Sheha Mjaja Juma, amesema mpango huo unaunga mkono juhudi za Serikali kupitia Green Legacy Program inayolenga kupanda miti milioni moja kwa mwaka.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira, Sheha Mjaja Juma.

Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) Suleiman Ali Mohamed,, amesema uhifadhi wa mazingira ni muhimu kwa mustakabali wa utalii, kwani rasilimali za asili ni sehemu muhimu ya vivutio vya Zanzibar.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Waendeshaji wa Utalii Zanzibar (ZATO), Suleiman Ali.