Zenj FM

Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia yawafikia maelfu ya wananchi Zanzibar

12 June 2026, 14:38

Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Dk. Haroun Ali Suleiman akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni hiyo.

Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imechangia maendeleo ya wananchi kwa kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kisheria na kijamii. Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo iliwafikia zaidi ya wananchi 420,000 Zanzibar na kuwapatia msaada wa kisheria pamoja na ufumbuzi wa matatizo yao.

Na Berema Nassor.

Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Dk. Haroun Ali Suleiman, amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imekuwa chachu muhimu ya maendeleo kwa wananchi kwa kusaidia kutatua kero na changamoto mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni hiyo, alisema awamu ya kwanza iliweza kuwafikia zaidi ya wananchi 420,000 Zanzibar, ambao walipata fursa ya kupata msaada wa kisheria na ufumbuzi wa changamoto zao.

Amesema kupitia kampeni hiyo, wananchi wengi nchini Tanzania wameweza kupata msaada wa kufuatilia na kutatua migogoro yao ya kisheria na kijamii.

Dk. Haroun ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ili kupata huduma za kisheria na kutatua kero zao.

Sauti ya Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Dk. Haroun Ali Suleiman.

Uzinduzi wa awamu ya pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia unatarajiwa kufanyika Juni 20, ukiwa na kaulimbiu: “Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo.”