Zenj FM

Kituo cha polisi Tumbatu kwa mara ya kwanza

13 August 2023, 4:08 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad (kushoto)akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi Daniel Shila wakikagua ujenzi wa kituo cha Polisi Tumbatu.Picha na Said Bakari

Kituo hicho cha polisi Tumbatu chenye hadhi ya daraja ā€œcā€ kinatarajiwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa kisiwa hicho.

Na Said Bakari.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema kukamilika kwa mradi wa kituo cha Polisi katika Kisiwa cha Tumbatu kutapelekea kutatua changamoto za Kiusalama katika kisiwa hicho.

Amesema hayo huko Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokua akikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi Tumbatu.

Amesema kituo hicho kitakapo kamilika kitaweza kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati na kwa urahisi kwani awali wanachi wa kisiwa hicho walikua wakifata huduma hio katika kituo cha Polisi Mkokotoni.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi Daniel Shila amesema kituo hicho kitapunguzia wanachi gharama wakati wanapo hitaji huduma za kipolisi hivyo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kuhakikisha wanaitunza miundombinu hiyo.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi Daniel Shila

Kwa upande wao wananchi wa Kisiwa hicho wameipongeza Serikali kwa kuwasogezea huduma hio karibu na wameomba Askari watakao pangiwa katika kituo hicho kitakapo kamilika wapatiwe makazi katika kisiwa hicho.

Sauti mwananchi wa Tumbatu