Zenj FM

Taka kuwa biashara Zanzibar

12 September 2023, 1:28 pm

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Muhammed Mussa aikiwa pamoja na washiriki wa mafunzo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Baraza la Jiji Michenzani Wilaya ya Mjini. Picha na Mary Julius.

Timu ya wataalam kutoka Jumuiya ya Mameya wa Afrika ya Kusini (AMALI) wametoa mafunzo  namna ya kutenganisha taka ngumu na taka nyepesi.

Na Mary Julius.

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Muhammed Mussa amevitaka vikundi vya usafi kutenga fungu kwa ajili ya kukodi magari yatakayowezesha kufanikisha ukusanyaji wa taka.

Mstahiki meya ameyasema hayo katika mafunzo ya kuwajengea uelewa wenyeviti wa vikundi vya usafi na watendaji wa baraza hilo juu ya kuchakata taka yaliyotolewa na taasisi ya wanaharakati wa mazingira wa Nipe Fagio kutoka Dar es Salama na  wataalam kutoka Jumuia ya Mameya wa Afrika ya Kusini (AMALI)  katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za baraza la jiji Michenzani wilaya ya Mjini.

Amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika kuliweka jiji la Zanzibar safi ni usafirishaji  wa taka kutoka maeneo mbalimbali hivyo kukodishwa kwa gari  hizo  kutasaidia usafirishaji wa taka kutoka majumbani na kuzipeleka maeneo yanayostahili lengo likiwa ni kuliweka jiji la Zanzibar safi na salama.

Sauti ya Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Muhammed Mussa

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Jiji Zanzibar kupitia huduma za jamii, Abdullatif Omar Haji amesema  kutokana na changamoto ya ulipaji wa taka kwa baadhi ya wananchi wataishauri serikali kuandaa utaratibu wa kulipisha ada ya taka kwa kupitia bili za Zeco.

Sauti ya mahojiano ya Mwenyekiti wa Baraza la Jiji Zanzibar kupitia huduma za jamii, Abdullatif Omar Haji na mtangazaji wa Zenj Fm, Ivan Mapunda.

Nao wadau kutoka Dar es Salaam wa taasisi ya  Nipe Fagio wamesema lengo la kuja Zanzibar  ni kuhakikisha wanatoa elimu ya uchakataji wa taka pamoja na kuandaa sehemu itakayotumika kupokea taka kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Zanzibar ili kufikia taka sifuri .

Sauti ya Matha Jumanne Masoud Kutoka Tasisi ya Nipe Fagio.