Zenj FM

Moto wateketeza hotel Pongwe

8 August 2023, 12:39 pm

Eneo la nje lililo ungua la hotel ya Karibu Beach Resort Pongwe. Picha na Fatuma

Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja amewataka zimamoto kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa wananchi.

Na Fatuma

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid  ameziagiza mamlaka ya zima moto, shirika la umeme na idara ya maafa  kuandaa utaratibu wa  kutoa elimu  ya  mara kwa  mara juu  ya mbinu za   kukabiliana  na majanga ya moto  kwa wawekezaji   wa hoteli za kitalii  ili kupunguza  adhari  zitokanazo na majanga hayo.

Mkuu wa mkoa Hadid ameyasema hayo huko kijiji  cha   pongwe  pwani  wilaya ya kati  wakati wa ziara  ya kuwafariji wamiliki wa hoteli  ya Karibu Beach Resort  iliyopatwa   na janga la kuunguliwa  na  moto  na kusababisha hasara   baada ya  kuungua  moto  sehemu  za jikoni ,sehemu ya kupokea wageni , paa,na baadhi ya vyumba  vya hoteli hiyo.

Eneo la ndani lililoungua la hotel ya Karibu Beach Resort

Amesema  hatua  hiyo  itasaidia  kutambua  mbinu  na hatua zinazofaa kuchukuliwa  pale mara  majanga yanapotekezea  hali iyayopelekea  kupunguza   hasara  kwa kiasi kikubwa kwa wawekezaji  zitokanazo na  majanga  hayo  ikiwemo  usalama wa wageni na mali zao pamoja na wafanyakazi.

Aidha amemtaka   mmiliki wa hoteli hiyo kua na moyo  wa subira  na serikali  iko pamoja  na wawekezaji wote  na hasa  wanaopatwa  na  majanga kama  hayo huku akiwasisitiza kua  makini  wakati  wa kutumia  vifaa  vinavyotumia nishati ya umeme na  gesi  ili kujikinga  na majanga  hayo  hasa katika kipindi hicho  cha upepo mkali.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Hadidi Rashid Hadidi

Kwa upande wake Kamanda wa polisi  mkoa wa kusini unguja Gaudianus .f. Kamugisha amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa kukabiliana na maafa  watahakikisha  wanakaa pamoja   kuandaa mikakati madhubuti itakayosaidia  kudhbiti  majanga hayo  ambayo yamekua yakiendelea kuzofisha  hali ya ukuaji wa uchumi wa wawekezaji  na taifa kwa ujumla.

Sauti ya Kamanda wa polisi  mkoa wa kusini unguja Gaudianus .f. Kamugisha