Zenj FM

Kijana ajinyonga Pemba

27 August 2023, 3:21 pm

Mwili wa marehemu Moh’d Omar Juma ukipandishwa kwenye gari.

Na Is-haka Mohammed

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina Moh’d Omar Juma maarufu Magodoro   anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 mkaazi wa Machomanne Kilimo amefariki dunia baada ya kuonekana akining’inia katika chumba kwa kujinyonga.

Khamis Issa Moh`d ni Mwanafamilia  wa marehemu amesema kijana wao huyo aliingia na kujifungia ndani ya chumba siku ya Ijumaa majira  saa nne za asubuhi lakini hakutoka na ndipo ndugu zake walipomgongea usiku lakini hakufungua mlango na walimwacha kwani kwa siku za hivi karibuni ilionekana hiyo kuwa ni kawaida yake.

Amesema ilipofika asubuhi ya  Jumamosi na kuona bado hajafungua ndipo walipoamua kuuvunja mlango na kumuona ameshafariki kwa kujinyonga akitumia kanga aliyoifungwa juu ya feni.

Sauti ya Mwanafamilia  wa marehemu Khamis Issa Moh`d .

Naye ndugu wa marehemu Moh`d, ambaye ni Nassor Omar Juma amesema kaka yake kwa masiku ya hivi karibuni alikuwa ni mgonjwa wa wasiwasi ambapo walifanya juhudi za kupelekea hadi katika hospitali ya afya ya akili Kidongo Chekundu Unguja na baada ya kuonekana hana tatizo katika afya ya akili walirudi naye na kuendelea kuishi nae kwa ukaribu.

Sauti ya Nassor Omar Juma ndugu wa marehemu

Akizungumzia tukio hilo Sheha wa Shehia ya Wara Massoud Moh’d amesema alipokea taarifa za kujinyonga marehemu Moh`d alipofuatwa na ndugu yake akiwa nyumbani kwake kwa ajili ya kutoa taarifa na yeye alichukua hatua ya kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Sauti ya Sheha

Marehemumu Moh`d aliwahi kuwa na mke ambaye waliachana na alibahatika kuzaa naye watoto watatu na tayari mwili wake umeshahifadhiwa katika makaburi ya kijijini kwao Dutani.