Zenj FM

Wanafunzi Pemba watakiwa kuitumia mitandao vizuri

6 October 2023, 2:35 pm

Wanafunzi wa Skuli ya Skondari ya Samia Suluhu Hassan na wenzao wa skuli ya Msingi Mwambe wakiwa katika mafunzo ya kutumia mtandao. Picha na Is haka Mohammed

Shirika la Save the Children Tanzania limetoa mafunzo kwa wanafunzi kisiwani pemba kwa lengo la kuwawezesha kupelekea ujumbe wao kwa viongozi wenye mamlaka kupitia jukwaa hilo la mikutano ya mtandaoni.

Na Is-haka Mohammed.

Kuwepo kwa jukwaa la kuwasiliana mtandaoni kumeelezwa kutawasaidia watoto katika kuwasilisha changamoto zao ili ziweze kuchukuliwa hatua kwa haraka na walengwa ikiwemo masuala yao ya kudai haki zao za kimsingi.

Hayo wameyaeleza wanafunzi wa Skuli za Samia Suluhu Hassan na Mwambe Wilaya ya Mkoani Pemba, wakati wakizungumzia mafunzo ya kuwasiliana Mtandaoni(Zoom Meeting) yaliyotolewa na Shirika la Save Tha Children Tanzania kwa wanafunzi hao ikiwa ni katika kujenga jukwaa la kuwasiliasha maoni ya watoto kupitia mikutano ya Mtandaoni.

WaKizungumza baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa kupitia njia hiyo ya matumizi ya mtandao itakuwa rahisi  kwao kama watoto kuweza kuwasilisha maoni yao ikiwemo yale ya kudai haki kwa mamlaka za juu ambao kuwapata kukaa maza moja inaweza kuwa shida kwa wanafunzi na watoto wengine.

Sauti ya wanafunzi wa Skuli za Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Kulinda na kutetea Haki za mtoto kupitia shirika la Save the Childen Unguja Pius Ulaya amesema teknojia ya mtandao endapo itatumika vyema itawawezesha  watoto kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na viongozi wao ili kuwasilisha madai juu ya haki zao ambazo zinakosekana.

Sayuti ya Mratibu wa Mradi wa Kulinda na kutetea Haki za mtoto kupitia shirika la Save the Childen Unguja Pius Ulaya.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo Pemba Micheal Mwalupale amesema kupitia fursa za kujieleza kwa watoto hao kwa viongozi wenye mamlaka itakuwa rahisi kwa watoto hao kuzipata haki zao kwa urahisi na kwa wakati.

Sauti ya Mratibu wa Mradi huo Pemba Micheal Mwalupale.