Zenj FM

Bei elekeze ya sukari yawaibua wafanyabiashara wa soko la Mwanakwerekwe

23 March 2024, 5:20 pm

Picha na Suleiman Abdalla.

Na Rahma na Suleiman

Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar kupitia waziri wa Wizira ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar Omar Shaaban ilitoa bei elekezi ya sukari ikiwa ni sh 2650 kwa kilo kwa upande wa unguja na sh 2700  kwa upande wa pemba.

Wafanyabiashara wadogo wadogo soko la Mwanakwelekwe wamewaomba wauzaji wa jumla kuifuata bei elekezi ya sukari iliyo pangwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar.

Wakizungumaza na zenji fm wafanyabiashara hayo wamesema bei wanayoinunulia sukari kutoka wafanya biashara wa jumla ni sh 13800 kwa kilo hamsini kwa nyeupe na nyekundu ni sh 12500 kwa polo, bei hiyo imepelekea kutokuwa na tija kwa wafanyabiashara hao hali ambayo inakwamisha kufikia bei elekezi ya sukari iliyo pangwa na serikali.

Aidha wafanyabiashara hao ameiomba serekali kusimamia  bei elekezi hususa kwa upande wa matajiri ili kuondosha kadhiia hiyo na kuwachukulia hatua wale wote wanaoficha sukari.

Sauti ya wafanyabiashara soko la Mwanakwerekwe.

Akizungumza kwa jia ya simu, Mkurugenzi Mkuu Tume ya Ushindani Halali Zanzibar Mohd Sijaamini amesema sababu inayopelekea mfumuko wa bei ya sukari ni kutokana na kuongezeka kwa gharama ya usafirishaji, kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo njee ya nchi pamoja na kuwepo kwa uzalishaji mdogo wa sukari katika kiwanda cha Mahonda.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu Tume ya Ushindani Halali Zanzibar Mohd Sijaamini