Zenj FM

Wafanyabiashara Pemba walalamikia kodi kubwa

22 September 2023, 5:01 pm

Moja katika ya maduka yaliyopo mjini Chake Chake Pemba ambapo baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wameeleza juu ya kodi kuwa kubwa na ugumu  wa biashara kwa sasa. Picha na Is-haka Mohammed.           

Wafanyabiashara kisiwani Pemba wameiomba serikali kuwapunguzia kodi ili kuweza kunusuru biashara zao.

Na Is-haka Mohammed.

Wafanyabiashara kisiwani Pemba wamedai kuwepo kwa kodi kubwa kunatishia uhai wa biashara zao na kuiomba serikali kuangalia upya hali ya kodi wanazotoza ili kunusuru hali hiyo isitokee.

Wafanyabiashara hao wameyasema hayo huko Chake Chake Pemba wakati wakizungumzia ugumu wa biashara zao unaosabishwa na kodi wanazotozwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) pamoja na taasisi zingine za serikali.

Wakizungumzia hali hiyo mfanyabiashara Rashid Nassor Moh`d (Manyimbo) na mwenzake Waziri Salim Waziri wamesema hawakatai kulipa kodi lakini wamekuwa wakishindwa kufuatia hali ngumu ya biashara na kuwepo kwa kodi isiyo rafiki kwao.

Sauti ya wafanyabiashara wa Chake Chake Pemba.

Naye Mkurugenzi wa ZRA Pemba Jamal Hassan Jamani amesema kodi ambazo wamekuwa wakitozwa wafanyabiashara hao ni makusanyo kutoka kwa  wananachi ambao ndio wanaolipa kodi hizo na pia ameeleza kuwa kodi zinazotozwa zimegawiwa kwa mujibu wa hali za biashara husika.

Sauti ya Mkurugenzi wa ZRA Pemba Jamal Hassan Jamani.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  ya Mamlaka wa Mapato Zanzibar ZRA Profesa Hamed Rashid Ikmany aliwataka wafanyakazi wa ZRA kuhakikisha lengo la ukusanyaji wa mapato waliloekewa linafikiwa na kutumia busara katika kutekeleza majukumu yao

Sauti ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  ya Mamlaka wa Mapato Zanzibar ZRA Profesa Hamed Rashid Ikmany.