Zenj FM

Jeshi la polisi Kusini Unguja kuimarisha ulinzi, usalama

12 March 2024, 5:15 pm

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja SACP Daniel Emanuel Shillah,

Na Mary Julius.

Katika kuhakikisha wananchi wanaofanya ibada za usiku katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan wanakuwa salama, Jeshi la Polisi laahidi kulinda watu na mali zao.

Jeshi la polisi mkoa wa Kusini Unguja limejipanga kuimrisha ulinzi na usalama kwa wananchi hasa katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja SACP Daniel Emanuel Shillah, ameyasema hayo wakati akizungumza na Zenji Fm na kuongeza kuwa katika kipindi hiki cha Ramadhan wannchi wengi huwa wanafanya ibada za usiku hivyo jeshi limejipanga kufanya doria ili kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada na majumbani.

Akizungumzia usalama barabarani kamanda Shillah amewataka madereva  kufuata sheria za usalama barabarani ili kuweza kujikinga na ajali zinazosababishwa na kutofuata sheria.

Aidha kamanda amewaomba wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuweza kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani.