Zenj FM

Kamishna wa Polisi Zanzibar atoa onyo wanaobambikia watu kesi

24 September 2023, 6:07 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad, akikagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Kituo cha polisi Mkoani. Picha na Omary Hassan.

Ujenzi wa kituo cha Mkoani umekuja kufuatia kuchakaa kwa kituo cha polisi Mkoani ambacho kimerithiwa tokea wakati wa ukoloni na kinatumika hadi sasa.

Na. Omary Hassan

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia vituo vya polisi kushtaki kesi za uongo kwa lengo la kukomoana.

Akikagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya la kituo cha polisi Mkoani, katika wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba ambacho kimegharimu kiasi cha shilingi milioni mia saba, amesema wapo baadhi ya watu hutumia askari wa jeshi la polisi wanaofahamu kufungua kesi za uongo na kesi za madai jambo ambalo ni kinyume na taratibu.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad

Kwa upande wake Fundi Mkuu wa ujenzi wa kituo hicho Omary Khamis amesema wanatarajia kumaliza na kukikabidhi kituo hicho baada ya wiki mbili zinazofuata.

Sauti ya Fundi Mkuu wa Ujenzi wa kituo hicho Omary Khamis