Zenj FM

Wafanyakazi ZAWA walipwa malimbikizo ya madeni ya mshahara

29 March 2024, 6:22 pm

Katibu Mkuu Chama Cha Wafanyakazi Wa  Huduma Za Umaa ZAPSWU Mwatoum Khamis Othman akiwa na viongozi wa ZAPSWA. Picha na Mary Julius

Viongozi wa chama cha wafanyakazi wa huduma za umma ZAPSWU na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha walikutana mwezi march mwaka 2024 na kukubaliana utekelezaji wa malipo ya deni hilo.

Mary Julius.

Zaidi ya wafanyakazi 560 wa mamlaka ya maji Zanzibar Zawa wanatarajiwa kulipwa malimbikizo yao ya madeni ya mshahara ya mwaka 2017-2018.

Katibu Mkuu Chama Cha Wafanyakazi Wa  Huduma Za Umaa ZAPSWU Mwatoum Khamis Othman ameyasema hayo wakati Akizungumza na waandishi wa habari kikwajuni  Zanzibar, amesema deni la malimbikizo ya tofauti za mshahara ya wafanyakazi wa ZAWA lilianza April 2017 mpaka June 2018 baada ya serikali kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wote ambapo kwa upande wa wafanyakazi wa ZAWA nyongeza ya mshahara ilianza kulipwa 2018 badala ya kulipwa 2017.

Aidha Katibu Mkuu Mwatoum Amesema katika kipindi chote hicho chama cha wafanyakazi wa umaa kimeendelea na mkakati wa kufatilia suala hilo kwa kufanya vikao mbalimbali ambapo wamekubaliana kuwalipa kwa  awamu mbili kwa asilimia 50 kila mwaka kuanzia  2023-2024  hadi 2024-2025 ambapo deni hilo linatarajiwa kumalizika. 

Sauti ya Katibu Mkuu Chama Cha Wafanyakazi Wa  Huduma Za Umaa ZAPSWU Mwatoum Khamis Othman

Nae  Katibu wa Kanda ya Unguja Mnyanja Simai Daima amesema utekelezaji huo utawahusu hata wale waliokuwa kazini kwa kipindi hicho na kwa sasa  wamesha staafu ambapo mchakato huo utapitia kwa akaunti zao za pencheni na kwa marehemu fedha hizo zitapelekwa Kamishani ya Wakfu na Mali ya Amana na warithi wataenda kuchukua haki yao.

Sauti ya Katibu wa Kanda ya Unguja Mnyanja Simai Daima