Zenj FM

Mratibu vikoba Unguja awataka wanawake kuchukua mikopo kwa malengo

7 April 2024, 6:27 pm

Mratibu wa vikoba unguja Catherine Marco Ifanda (kati) akiwa na mwenyekiti wa st joseph mama’s na katibu kulia. Picha na mwandishi wetu.

Na Mary Julius.

Mratibu wa vikoba Unguja Catherine Marco Ifanda amewataka akinamama wanaojiunga kwenye vikundi vya vikoba kuchukua mikopo kwa malengo ya kujiendeleza.  

Mratibu ameyasema hayo katika sherehe ya kuvunja  kikoba cha St Joseph Mamas  hafla iliyofanyika katika ukimbi wa Upendo House  Kiponda wilaya ya Mjini Zanzibar.

Amesema vikoba vimewasaidia akinamama katika kupata mitaji ambayo imewasaidia katika kujiendeleza na kuijenga familia kiuchumi.

Aidha Katibu amekemea  tabia za kuchukua mikopo ambayo mwanakikundi hana malengo nayo hali  inayopelekea kukosekana kwa marejesho na hatimaye kuingia katika migogoro ya kiuchumi.

Sauti ya Mratibu wa vikoba unguja Catherine Marco Ifanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha st joseph mama’s Rose Haule amesema kikundi hicho kumewasaidia wakinamama hao kujenga umoja na mshikiano pamoja na kujikuza kiuchumi kwa mtu mmoja moja na family kwa ujumla.

Sauti ya Mwenyekiti wa kikundi cha St Joseph mama’s Rose Haule.

Nao wanachama wa st joseph mamas wamesema ndani ya miaka miwili wameweza kufanya mambo mengi ya maendeleo ambayo kama wasingekuwa ndani ya kikundi hicho wasingeweza kuyafanya ikiwemo kununua viwanja, kusomesha watoto na kupata mitaji ya biashara.

Sauti ya wanachama.

Zaidi ya sh milioni 40 zimegwanywa kwa wanaKikundi wa kikundi cha  st Joseph Mama’s.