Zenj FM

Mbunge Pondeza ahimiza kusaidia wasiojiweza

30 March 2024, 6:06 pm

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza (aliyevaa kanzu) akikabidhi msaada wa futari kwa uongozi wa skuli ya Dkt Salmin Amour. Picha na Suleiman

Na Suleiman

Mbunge wa jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza  amezitaka taasisi na wahisani kutoa sadaka katika mwezi mtukufu wa ramadhan na kuwasaidia wasiokuwa na uwezo ili kujipatia fadhila zinazopatikana katika mwezi huo.

Mbunge Pondeza ameyasema hayo mara baada ya kuwapatia futari wanafunzi waliopo kambi katika skuli ya Dkt Salmin  Amour,amewataka wanafuzi hao kuengeza pidii ili kuleta ufaulu mzuri katika masomo yao.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza

Kwa upande wake  Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Dkt Salmin Amour , Tifly Mustafa Nahoda amempongeza Poteza kwa jitihada anazozifanya mara kwa mara kwa kuwapatia misaada katika skuli hiyo

Aidha Mwalimu Mkuu Tifly Mustafa ameahidi kuleta matokeo mazuri kwa wanafunzi hususa kwa kidato cha nne na sita.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Dkt Salmin Amour , Tifly Mustafa Nahoda

Nae rais wa wanafunzi wa skuli ya dkt Salmin Amour, Abdul, Rahman Haji Mussa ameahidi kuleta matokeo mazuri na kuifanya skuli yao kuwa skuli bora.

Sauti ya mwanafunzi AbdulRahman Haji Mussa

Sadaka zilizo tolewa ni pamoja na vipolo vya magharage ,sukari , mchele, unga wa ngano na mafuta.