Zenj FM

Maafisa TRA, ZRA wafundwa Zanzibar

15 August 2023, 5:35 pm

Maafisa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA wakifuatilia moja ya mada zilizowasilishwa kwenye Semina.

Na Ahmed Abdullah

Maafisa kodi wa mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA na mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wametakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wateja ili kuwa na mahusiano mazuri baina ya mlipakodi na mamlaka hizo.

Naibu kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ofisi ya Zanzibar Saleh Haji Pandu wakati akifungua semina elekezi kwa maafisa hao juu ya marekebisho ya sheria za kodi huko Ofisi za TRA, Kinazini Zanzibar ambapo amesema hatua hiyo itawapa ari walipakodi hao katika kuwasilisha kodi zao.

Aidha amewasisitiza maafisa hao kufanyakazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Sauti ya Naibu kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ofisi ya Zanzibar Saleh Haji Pandu.

Kwa upande wake Afisa mkuu wa elimu na mawasiliano kwa walipakodi kutoka TRA Dkt. Shuwekha Salum Khalfan amesema marekebisho ya sheria za kodi yanayofanywa mara kwa mara ni kutokana na serikali kupokea maoni juu ya changamoto zilizopo katika sheria hizo hivyo marekebisho hayo hupunguza changamoto hizo na kuweka mazingira bora ya ulipaji kodi.

Sauti ya Afisa mkuu wa elimu na mawasiliano kwa walipakodi kutoka TRA Dkt. Shuwekha Salum Khalfan.

Nao washiriki wa semina hiyo wamesema simina hiyo ita wasaidia kupanua wigo wa utendajikazi na kutoa huduma bora kwa walipakodi.

Sauti ya washiriki wa semina.