Zenj FM

Sheha Mwembeshauri alia na uchafu katika eneo la jumba namba 2

24 April 2024, 4:56 pm

Hili ni eneo la jumba namba mbili picha na Suleiman

Na Suleiman na Rahma.

Jumba namba 2 na namba 1 yapo katika shehia ya mwembeshauri wilaya ya mjini, haya ni majumba ya ghorofa ambayo yalijengwa enzi za Rais wa kwanza wa Zanzibar.

Sheha Wa  Muembe Shauri Abdalla Ali Abdalla amewataka wakazi wa jumba namba moja na  namba mbili  michenzani kuacha kutupa taka ovyo na kutoa mashikiano ya kufanya usafi katika eneo lao.

Akizungumza na Zenji Fm amesema wakaazi wa jumba namba 1 na jumba namba 2 wamekuwa na tabia ya kutupa taka ovyo katika maeneo yanayo zunguka jumba hili hali inayopelekea kuwaathiri wapiti njia na watu wanaoishi katika nyumba za chini.

Aidha sheha amesema wakazi hao  wamekuwa wakifanya uharibifu wa miundombinu ya maji katika eneo hilo ,

Sauti ya Sheha Wa  Muembe Shauri Abdalla Ali Abdalla.

Nae Diwani wa wadi ya Rahaleo jimbo la Kikwajuni Mbaruk Hanga amethibitisha kuwepo kwa changamoto ya jaa lisilorasmi pamoja na kutokuwepo kwa mashirikiano na wananchi hao.

Aidha amewataka wakaazi hao kuwa na mashirikiano na viongozi pamoja na kuweka mazingira safi ili kuepuka maradhi ya mripuko.

Sauti ya Diwani wa wadi ya Rahaleo Mbaruk Hanga.