Zenj FM

Maofisa wa vyuo vya mafunzo Pemba watakiwa kubadilika

29 August 2023, 2:50 pm

Maofisa wa Chuo cha Mafunzo kutoka kambi mbalimbali kisiwani Pemba wakiwa kwenye mafunzo ya mwongozo wa kutoa malalamiko vizuizini huko katika makao makuu ya chuo cha mafunzo Pemba- Wete.

Na Is-haka Mohammed Pemba.

Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzania umesema mwongozo wa malalamiko katika vizuizi (Vyuo vya Mafunzo) umewekwa  kwa ajili ya kusaidia utatuzi wa changamoto na malalamiko ya walio vizuizini ili kutoa nafasi ya kushughulikiwa na taasisi zinazohusika.

Mratibu wa Mtandao huo Zanzibar Suleimana Mujuni Baitani amewataka kuwahamasisha watu walio vizuizini kuzijaza fomu hizo za malalamiko kupitia mwongozo huo kwani kutatoa fursa kwa tume iliyotajwa na Mwongozo kutekeleza  wajibu kwa ufanilisi.

Baitani ameyasema hayo wakati wa uwasilishaji wa Utoaji wa Mafunzo juu ya Mwongozo wa Malalamiko na Mawasiliano Vizuizini kwa maofisa wa Vyuo vya Mafunzo Pemba yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Vyuo hivyo Wete Pemba.

Sauti ya Mratibu wa Mtandao huo Zanzibar Suleimana Mujuni Baitani

Akiwasilisha mwongozo huo kwa maofisa wa vyuo vya mafunzo Pemba Mkuu wa Idara ya Sheria na Urekebishaji Chuo Cha Mafunzo Zanzibar ACP Seif Makungu amesema mantiki ya mwongozo huo ni kuwawezesha wanafunzi kuwasilisha malalamiko yao.

Kwa upande wao maofisa wa vyuo vya mafunzo Pemba wameahidi kuufanyia kazi mwongozo huo pamoja na kushauri ushirikiano kwa kila hatua kwa taasisi zinazohusika.