Zenj FM

Tamwa Zanzibar yawanoa waandishi wa habari Pemba

25 August 2023, 3:56 pm

Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa Zanzibar Saphia Ngalapi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kisiwani Pemba katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu uandishi bora wa Habari.Picha na Is-haka Mohammed

Waandishi wa Habari Pemba wanatakiwa kufanya uchunguzi yakinifu kabla ya kurusha hewani habari za  udhalilishaji.

Na Is-haka Mohammed Pemba.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa Zanzibar) kimewakumbusha waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kuandika habari zenye tija na kupelekea mabadiliko ya kweli kwenye masuala ya kukabiliana na matendo ya udhalilishaji wa kijinsia.

 Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Utetezi Tamwa Zanzibar Saphia Ngalapi ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu yaliyolenga kuwapiga msasa waandishi habari 16 wa kisiwani Pemba juu ya kuandika kwa uweledi habari zinazohusu udhalilishaji yanayoendelea katika ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake Chake.

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa kwa waandishii wa habari kuandika habari  habari bora kwa kufuata maadili za udhalilishaji ambazo zitasaidia katika kuleta mabadiko chanya kwa jamii na taasisi mbali mbali.

Sauti ya Mkuu wa Mawasiliano na Utetezi Tamwa Zanzibar Saphia Ngalapi.

Naye Mwenyezeshaji katika mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Aimani Duwe amesema sifa moja ya mwandishi wa habari ni kuwa mbunifu na kuwataka kuwa wabunifu wanapoandika habari zinazohusu uhdalilishaji wa kijinsia.

Sauti ya Mwezeshaji Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Aimani Duwe.