Zenj FM

Zaidi ya wajawazito elfu mbili wafikiwa na M-MAMA Zanzibar

25 April 2024, 5:48 pm

Waziri wa afya Nassor Ahmed Mazrui (aliye simama) akizungumza katika kikao kazi cha kujadili mpango wa kuendeleza M-MAMA Zanzibar.

Mary Julius.

Wananchi wametakiwa kushirikiana na wizara ya afya katika kuwahimiza wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Waziri wa afya Nassor Ahmed Mazrui ameyasema hayo  alipokuwa akizungumza katika kikao kazi cha kujadili mpango wa kuendeleza M-MAMA Zanzibar uliowashirikisha Wataalamu na wadau mbalimbali ambapo amesema kuwa Vifo vingi vya mama na mtoto vinatokana na baadhi ya

Kinamama kutohudhuria klinik na hospitali wakati wa Kujifungua hali inayosababisha matatizo ikiwemo kifo.

Sauti ya Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui

Mwenyekiti wa kikosi kazi cha M-MAMA Zanzibar Mohamed Habib amesema mpango huo unalengo la kuhakikisha vifo Vya mama na mtoto vinapungua iwapo utatumika vizuri.

Sauti ya Mwenyekiti wa kikosi kazi cha M-MAMA Zanzibar Mohamed Habib

Rahma Bajuni ni msimamizi wa mpango wa M- MAMA kitaifa Kutoka vodafone amesema ni wajibu wa kila mwanafamilia Kuhakikisha anatumia mpango huo ili kumuwahisha mama Na mtoto kuokoa maisha yao.

Sauti ya Rahma Bajuni ni msimamizi wa mpango wa M- MAMA kitaifa Kutoka vodafone

Disemba 2022 Zanzibar ilianza rasmi kutumia mpango wa M-MAMA na hadi kufikia 2024 zaidi ya mama na watoto elfu Mbili walisafirishwa kupitia mpango huo.