Zenj FM

Jamii yatakiwa kuona umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari

11 March 2024, 5:12 pm

Wananchi waliojitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari bungi

Na Mary Julius.

Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed  Mahamoud  amesema  serikali inahitaji kuwa na akiba ya kutosha ya damu salama ili kuokoa maisha ya watu pale wanapokabiliwa na majanga.

Akizungumza katika zoezi la uchangiaji damu huko  kiwanja cha Bungi  Wilaya ya Kati Ayoub  amesema hatua hiyo ni kuwahakikishia usalama  wale wote wenye mahitaji ya damu salama  hasa wanapopatwa na ajali na mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Baadhi ya wananchi walio jitokeza katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari bungi wilaya ya kati

Aidha amesema serikali kupitia kitengo cha damu salama na taasisi nyengine  itaendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu  ili kuwa na akiba ya kutosha ya damu salama hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Mkuu wa mkoa wa kusini Unguja Ayoub Mohamed  Mahamoud.

Naye  Mkugenzi matukio  wa  ZBC   Salum Ramadhan Abdalla  na  Afisa  uhusiano wa kitengo  cha damu salama  Ussi Bakari Mohamed  Wamesema wameanzisha kampeni hiyo ya Mwavuli wa damu salama  ili  kusaidia  makundi   mbali mbali ya jamii na kupongeza ushiriki mkubwa wa wananchi  katika zoezi hilo ambapo kampeni hiyo imelenga kupata chupa mia sita na hamsini kwa Mkoa huo.

Sauti za Mkugenzi matukio  wa  ZBC   Salum Ramadhan Abdalla  na  Afisa  uhusiano wa kitengo  cha damu salama  Ussi Bakari Mohamed

Nao wananchi walioshiriki katika zoezi la uchangiaji damu Ramadhan Pandu Haji na ndugu Munira Mmanga Mohd wamesema ni vyema kwa jamii ikaona umuhimu wa suala la kuchangia damu kwa hiari ili kuwasaidia wagonjwa watakaokuwa na mahitaji nchini.

Sauti za wananchi walioshiriki katika zoezi la uchangiaji damu.