Zenj FM

Wanafunzi wa kiume wilaya ya Kati Unguja wapewa mbinu kufikia ndoto zao

10 September 2023, 1:47 pm

Afisa Elimu wilaya ya Kati Unguja Somoe Said Mussa akimtunuku Cheti mmoja kati ya washindi 20 wa mbio za marathoni kilomita nne 4 kwa Skuli 15 za Wilaya ya hiyo. Picha na Hakika Mwinyi.

Na. Hakika Mwinyi

Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Somoe Said amewataka wanafunzi wa kiume kujiepusha na vishawishi ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.

Afisa Elimu ameyasema hayo katika ghafla ya kuwatunuku vyeti wanafunzi Wakiume 20 walio shiriki katika marathon iliyo andaliwa na Taasisi ya Happy Teenagers Talk, hafla iliyofanyika katika uwanja wa ofisi za Wilaya Dunga Wilaya ya Kati Unguja, Amesema maisha ya yanachangamoto nyingi ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya  vitendo vya udhalilishaji,  mimba za utotoni.

Aidha Amesema taasisi nyingi zimekuwa zikijikita katika kuwaelimisha watoto wa kike na kuwasahau watoto wa kiume hivyo ameipongeza taasisi ya  happy tennega  kwa kuwaaamua kuwaelimisha watoto  wa kiume ili waweze kujitambua na kuachana na vitendo viovu.

Sauti ya Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Somoe Said.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Happy TeenagersTalk Happiness Johnson Mwita amesema lengo la kuanda Marathoni kwa wanafunzi hao ni kuwaweka karibu na kuzungumza nao ili kuhakikisha vijana wanaepukana na vishawishi ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, ndoa za mapema na ngono zembe katika umri mdogo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Happy Teenagers Talk Happiness Johnson Mwita.

Nae Mwalimu wa Michezo kutoka Skuli ya sekondari Uzini  Ali Mabrouk Mshimba kwaniaba ya Walimu wenzake amewataka wazazi kuwahamasisha watoto kushiriki katika michezo.

Sauti ya Mwalimu wa Michezo wa Skuli ya Sekondari Uzini  Ali Mabrouk Mshimba.

Kwa uapande wake  mwanafunzi Bilali Abdallah Hassan kutoka Skuli ya Uzini ambae aliibuka mshindi wa kwanza katika mashindano hayo kwaniaba ya wenzake amewaomba  wanafunzi wenzake kutovunjika moyo, wazidishe jitihada  katika masomo.

Jumla ya zawadi za aina nne zimetolewa kwa washindi hao ikiwemo medali za dhahabu na Fedha, sturdy tour kwa washiriki ndani na nje ya Zanzibar, fedha taslim pamoja na vyeti kwa washiriki wote 159 wa skuli 15 za Wilaya ya Kati.