Zenj FM

Madereva wazembe kupokonywa leseni Zanzibar

2 May 2024, 2:24 pm

Mkaguzi msaidizi wa polisi Omar Hamad Omar (kulia) SGT Ali Abdlla C kati ) wakiwa ndani ya studio ya Zenj fm. Picha na Suleiman Abdalla.

Na Suleiman Abdalla

Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani watoa elimu ya usalama barabarani kupitia radio visiwani Zanzibar.

Kitengo cha Usalama Barabarani Zanzibar kimewataka madereva na watembea kwa mguu kufuata kanuni na sheria zilizowekwa ili kuepuka ajali za mara kwa mara.

Akizungumza katika studio za Zenji fm SGT Ali Abdlla amesema moja ya sababu zinazopelekeaa ajali za barabarani ni kutokufuata sheria na kupuuza alama za barabarani pamoja na kuendesha mwendokasi kinyume na sheria jambo ambalo linahatarisha maisha ya watumizi wa barabara

SGT Ali amesema atakae kiuka kanuni na sheria za barabarani adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kunyanganywa leseni na kurudishwa chuoni kwa lengo la kupatiwa tena elimu ya udereva pia amewataka madereva kufuata sheria kuepukana na adhabu hizo.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Omar Hamad Omar amesema Jeshi la Polisi limejipanga kufanya operesheni kubaini makosa yanayofanywa na madereva na kutoadhibu kwa mujibu wa sheria pamoja na kutoa elimu sehemu mbali mbali kwa  lengo la kufahamu matumizi na alama za barabarani.